Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, September 28, 2012

TAARIFA MUHIMU KUTOKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII...!

Na: Tulizo Kilaga

Wizara ya Maliasili na Utalii itawachukulia hatua wale wote watakaokiuka sheria, kanuni na taratibu zinazotawala utekelezaji wa mchakato wa kuwapata wawekezaji kwenye vitalu vilivyopo kwenye Maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori (WMAs).


Akifungua warsha ya mafunzo kuhusu mchakato wa kufungua maombi ya uwekezaji kwenye vitalu vya WMAs iliyofanyika katika Ukumbi wa Blue Peel jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Bw. Paul Sarakikya alisema mchakato husika utahusisha watu wenye uwezo wa fedha hivyo unaweza kusababisha uwepo wa mazingira ya rushwa.

Alisema mchakato huo ni nyeti na unahitaji uadilifu na umakini mkubwa katika kuutekeleza. Kushindwa kuzingatia vigezo vitakavyokubalika katika mchakato huo kutasababisha migogoro isiyo ya lazima hivyo kudhoofisha maendeleo ya Jumuiya na kukatisha tamaa vijiji vilivyotenga maeneo kuanzisha WMAs. “Napenda kusisitiza kuwa, Kanuni za WMAs zinazitaka Jumuiya kufanya uteuzi wa wawekezaji kwa kutumia vigezo vilevile vilivyotumiwa na Wizara kuwapata wawekezaji kwa kutumia vigezo vilivile vilivyotumiwa na Wizara kuwapata wawekezaji kwenye vitalu vyake.

Vigezo hivyo viko kwenye Kanuni za Uwindaji wa Kitalii (2010) kifungu cha 10(2). Hivyo washiriki watapata fursa ya kuvipitia na kuviwekea alama kwa kuzingatia mahitaji na hali halisi ya WMAs, alisema Bw. Sarakikya.Aliongeza kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii itashirikiana na vyombo vya dola kufuatilia utekelezaji wa mchakato huu na haitasita kuwachukulia hatua wale wote walioshindwa kuweka mbele maslahi ya Jumuiya zao na ya Taifa kwa Ujumla,” alisema Bw. Sarakikya. Bw. Sarakikya alisema kwa kutambua umuhimu wa mchakato wa ugawaji vitalu hivyo Wizara ya Maliasli na Utalii imetoa Afisa kutoka Kitengo cha Matumizi Endelevu ya Wanyamapori ili kutoa mafunzo. Hivyo Wizara inatarajia wajumbe wote watakubalina na kuhitimisha hatua za kimchakato zitakazotumika, na hatimaye kuwa na mwongozo utakaotumika na Kamati zitakazo fungua maombi hayo.


Warsha ya Mafunzo kuhusu Mchakato wa Kufungua maombi ya uwekezaji kwenye vitalu kwenye maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori imelenga kuwawezesha wajumbe kupata uelewa wa pamoja wa nini cha kufanya baada ya Jumuiya zilizo nyingi kuwa zimepokea maombi ya uwekezaji kwanye vitalu vya WMAs kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 na Kanuni za WMAs 2012.

No comments:

Post a Comment