Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, September 8, 2012

Wafichueni viongozi wanaoficha mali..

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala bora, George Mkuchika  amewataka watumishi wa Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma (Uchunguzi na Upelelezi) kuwa waadilifu na wazalendo katika kuwafichua viongozi wanaodanganya kuhusu mali wanazomiliki.

Mkuchika alisema hayo jana mjini Morogoro wakati akifungua mafunzo ya maofisa wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma.

“ Kazi ya uchunguzi na upelelezi ni nyeti kwani ina manufaa katika kuzuia vitendo vya ukiukwaji wa maadili hususan rushwa na matumizi mabaya ya rasilimali za umma, ili kazi hii iwe na manufaa ni lazima wachunguzi wawe waadilifu na wazalendo kwa nchi yetu,” alisema Mkuchika.

Alisema wachunguzi na wapelelezi wasipofanya kazi zao vyema, wanaweza kuwa chanzo cha kupoteza taswira ya taasisi kwa umma na taifa.

“ Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma wanatakiwa kutumia ujuzi wanaopata katika kuhakiki  mali wanazozitamka viongozi, na kuwafichua viongozi wote wanaoudanganya umma ili kujenga Taifa letu,”alisema.

Naye  Jaji mstaafu, Salome Kaganda ambaye ni Kamishna wa maadili alisema kuwa wamefanikiwa kuwapatia mafunzo ya kutosha watumishi wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kutumia  mbinu za kisasa za uchunguzi ambazo zitawasaidia katika kuboresha utendaji wa kazi.

“ Chuo cha maofisa wa polisi kimefanikiwa kufikia lengo kwa sababu, tumewafundisha mbinu za kisasa  hivyo kitawasaidia katika   kuboresha utendaji wa kazi,” alisema Kaganda.

Kaganda alisema kuwa, lengo  ni kuwapatia watumishi mafunzo endelevu ya uchunguzi katika ngazi za juu kutoka ngazi ya cheti hadi stashahada ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

No comments:

Post a Comment