Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, October 20, 2012

JWTZ WASAIDIA KUDHIBITI MAANDAMANO YA WAISLAM JIJINI DAR ...!


Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa katika Maeneo ya Kariakoo na viunga vyake kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika .


Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu.


Safari ya kuelekea Kituo Kikuu ilianzaAskari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wakimwingiza katika gari muumini wa Kiislamu aliyekamatwa katika viunga vya maeneo ya Ikulu


Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo


Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki
Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo


Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo leo


Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leoAskari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo


Magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara ya Msimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka kuandamana.

Watu hao walifika mmoja mmoja maeneo ya Ikulu kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.
 
Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha. Katika maeneo ya Kariakoo vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania vimekuwa vikifanya doria ili kuimarisha hali ya ulinzi.Picha kwa hisani ya Happiness Mnale

No comments:

Post a Comment