Mrembo wa Ilala, Magdalena Roy, usiku
wa kuamkia leo amefanikiwa kunyakua taji la mrembo wa pili kuingia
hatua ya nusu fainali ya Redd's Miss Tanzania 2012 baada ya kuwashinda
warembo wengine 29 na kutwaa taji la Top Model.
Magdalena aliibuka mshindi katika
shindano dogo la Redd's Miss Tanzania lililofanyika usiku wa kuamkia leo
katika Hoteli ya Kimataifa ya Naura Springs jijini Arusha.
Kwa matokeo hayo Top Model,
Magadalena Roy anaungana na Miss Photogenic, Lucy Stephano katika nusu
fainali hiyo na kukaa tayari kusubiri warembo wengine 13 watakaoungana
katika Nusu fainali hizo.
Taji la TOP MODEL lilikuwa linashikiliwa na mrembo wa Temeke, Mwajabu Juma.
Mrembo kutoka Mkoa wa Mara na Miss
Kanda ya Ziwa 2012, Eugene Fabian nae alifanikiwa kutwaa taji la Ubalozi
wa Hotel ya Naura Spring ya jijini Arusha.
Egene alitangazwa kunyakua taji hilo
usiku wa kuamkia leo wakati wa shindano dogo la Redds Miss Tanzania 2012
la kumsaka Top Model ambaye pia ataingia katika hatua ya 15 bora ya
Shindano hilo la taifa la Miss Tanzania. Awali taji la Balozi wa Naura
Spring Hotel lilikuwa likishikiliwa na Neema Joel.
picha zaidi zitawajia baadae kidogo.
No comments:
Post a Comment