Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 15, 2012

NSSF USA RIVER YAFUNGUA OFISI MPYA ARUMERU KUWASOGEZA WANANCHI KARIBU NA HUDUMA BORA...!

 
Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF Ramadhani Dau akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ofisi mpya ya mfuko huo katika eneo la Usa river Wilayani Arumeru.

Mkurugenzi mwendeshaji wa NSSF Cricentus Magori  (mwenye suti nyeusi ) na  katikati ni Mkurugenzi Mkuu Ramadhani Dau wakiingia katika eneo la uzinduzi.

Wadau mbalimbali, wafanyakazi na wanachama wa NSSF wakiwa ndani ya jengo hilo jipya ili kujionea namna ofisi zilivyokamilika tayari kwa huduma (Picha zote na Story Mahmoud Ahmad – Arusha).

Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) umezindua ofisi mpya katika kata ya Usariver wilayani Arumeru ikiwa ni moja kati ya kuboresha huduma za wanachama wake katika wilaya hiyo ili kuweza kuwasogezea huduma wananchi karibu zaidi.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF Bw. Ramadhani Dau amesema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya ambazo zinaiingizia michango mingi zaidi katika mfuko huo ambapo amesema kuwa kwa mwezi huingiza milioni 432 kwa mwezi.
Bw.Dau ameongeza kuwa mchango huo kwa mwezi ni mkubwa sana kwa kuwa ndani ya mwaka mzima ni sawa na shilingi biloni tano, hali mbayo inaashiria kuwa kukiwa na ofisi hiyo karibu kutaongeza idadi ya wananchama wengine wapya katika mfuko huo.
Aidha amefafanua kuwa lengo la NSSF kufungua ofisi hiyo ni kuwa karibu na wanachama ili waweze kuweka michango yao kwa urahisi zaidi na kuwapunguzia gharama za kufuatilia mafao ambapo hapo awali walikuwa wanalazimika kufuata huduma zote za mfuko mjini Arusha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Cricentus Magori amesema kuwa shughuli ambazo zinafanyika katika wilaya hiyo haswa mashamba makubwa ya maua ambayo yapo maeneo mbalimbali, shughuli za uchimbaji wa madini ndio chachu ya kupata michango mingi na wanachama wengi katika wilaya ya Arumeru.
Bw. Magori amesema kuwa kwa sasa wilaya hiyo ina wanachama elfu saba ambapo amesema kuwa wameona ni muhimu kufungua ofisi ili kuwapatia huduma na kuondoa usumbufu wa kufuata huduma hizo mjini Arusha.
Katika uzinguzi huo uliofana sana ulifanyika katika kata ya Usa River wilaya ya Arumeru na kuwashirikisha wafanyakazi na wanachama wa mfuko huo pamoja na wadau mbalimbali.

No comments:

Post a Comment