Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 15, 2012

SERIKALI YA TANZANIA KUWANYANG'ANYA WAWEKEZAJI VIBALI...!

Serikali inatarajia kuwanyang’anya wawekezaji waliopewa vibali vya kujenga hoteli za kimataifa kwenye hifadhi, kutokana na kushindwa kuendeleza maeneo hayo.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kuhusiana na kongamano la kwanza la Afrika, kuhusu usimamizi wa utalii endelevu katika hifadhi za taifa, litakaloanza Oktoba 15 na kushrikisha washiriki 412 toka nchi 40 za Afrika.
Alisema kuwa maeneo hayo walipewa kwa lengo la kuyaendeleza na kupunguza uhaba wa maeneo ya kufikia watalii, lakini wameyahodhi na kushindwa kuendeleza, jambo linalokera na kulazimisha serikali kuchukua hatua zingine.
“Tutayachukua maeneo haya na yatakuwa chini ya hifadhi husika, kisha tutawapatia wawekezaji  wengine kuwekeza katika maeneo haya, na tutatoa kipaumbele kwa wazawa,” alisema Nyarandu.
Alisema kuwa Tanzania inahitaji hoteli za kutosha, sababu inakabiliwa na uhaba mkubwa wa vitanda vya kulaza wageni na kutoa mfano wa Mkoa wa Arusha ambako kuna vitanda 2,800, Dar es Salaam 3,700, Mwanza 914 na Kilimanjaro 414, wakati mji wa Nairobi nchni Kenya una vitanda 15,000 na Mombasa na Malindi 28,000, idadi ambayo inavimeza vitanda vya hapa nchini.
Alisema ili kukidhi mahitaji yaliopo kwa sasa ambayo ni makubwa sana, kutokana na kupokea idadi kubwa ya watalii na hasa wakati wa Msimu wa Utalii, kunahitajilka jitihada za haraka kukidhi hilo.
Aidha, serikali inatarajia kufungua Uwanja wa Ndege wa Arusha Mjini, ili uweze kutumika kwa kuruka na kutua ndege za kutoka
Nairobi moja kwa moja bila kupitia KIA.
“Tukifungua Uwanja huu tutaweza kuongeza utalii kwa zaidi ya asilimia kumi, tena kwa haraka sana, hivyo tupo mbioni kuanza hili kwa ajili ya kupunguza pia muda mrefu wa kukaa watalii uwanja wa KIA kusubiri usafiri wa Nairobi,”alisema.
Kuhusu usalama wa watalii kutokana na mauaji ya watalii yaliyotokea siku za karibuni, alisema serikali wameongeza ulinzi wa kutosha maeneo ya hifadhi na kudhibiti wanaoingia bila sababu.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment