Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, October 21, 2012

TAHADHARI KUHUSU MABOMU ZAIDI YA 30 YALIYOTEGWA MAENEO YA MPAKA WA TANZANIA NA MALAWI....!

Kuna taarifa kwenye mitandao ya simu inayoendelea kutolewa kwenye message za simu kwamba  kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye uzito usiopungua tani 100 na kuwataka wananchi katika mikoa ya Tanzania iliyo jirani na Malawi kuwa waangalifu. 
 
Taarifa hiyo imetaka wenye wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige simu 0756000042. Taarifa hiyo imedai kwamba imetolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Tunapenda kutoa taarifa kwamba taarifa hizo siyo za kweli na lengo lake  haliwezi kuwa zuri kwa Watanzania.  Wananchi wanashauriwa kutotuma taarifa zozote kwenye namba hiyo ama kuziamini taarifa za aina hiyo.


Assah Mwambene
Mkurugenzi, Idara ya Habari Maelezo.

No comments:

Post a Comment