Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 19, 2012

WAJUMBE BARAZA LA WAWAKILISHI CCM WAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA ILI ZANZIBAR ISIWE NCHI YA MACHAFUKO....!

Wajumbe  wa Baraza la Wawakilishi (CCM) wamelaani vikali vitendo vinavyoendelea kufanywa na jumuiya ya mwamsho  kwa kuvunja amani, utulivu na kusababisha vurugu katika mji wa Zanzibar  kuanzia jana.
Hapo jana kundi la mwamsho lilivamia nyumba za watu, maduka  na kupora bidhaa kadhaa katika maduka  na kusababisha hasara kubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Mbweni kwenye ukumbi wa baraza la wawakilishi, Mhe. Hamza Hassan Juma kwa niaba ya wawakilishi wa CCM amesema  wakati umefika kwa serikali kuchukuwa hatua zinazofaa kabla hali haijawa mbaya zaidi, kwani kuendelea kukaa kimya kwa serikali kutatoa sura mbaya kwa wananchi.
Amesema serikali imeunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kuondoa  kasoro zilizokuwepo na kuwafanya wananchi  kuishi kwa amani na usalama na kuweza kuondoa tofauti zao za kisiasa.
Amesema isifike wakati Zanzibar ikawa kama  zile nchi zenye  machafuko na kuwafanya wananchi wake  kushindwa kuishi kwa amani na salama.
Hivyo wajumbe hao wameitaka serikali  mara moja kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika na ghasia hizo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment