Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, October 9, 2012

Wanafunzi 97 wazuiwa kufanya mitihani Kahama

Wanafunzi  97 wa shule ya sekondari ya Seeke, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, hawatafanya mitihani ya kumalinza kidato cha nne kutokana na kukosa fomu za maendeleo ya mwanafunzi akiwa shule ya msingi kuingia sekondari (TSM 9).

HaIi hiyo ilijitokeza jana wakati wanafunzi hao wakiwa shuleni wakisubiri kuingia katika vyumba vya mitihani na kuzua utata mkubwa baina ya uongozi wa shule na watahinwa hao.

Wakizungumza na NIPASHE, wanafunzi hao walisema fomu hizo walizijaza na kila mwanafunzi alilipa ada ya mitihani, lakini walishangaa kuona jana wakizuiwa kuingia katika chumba cha mtihani kufanya mitihani.

Walisema ni wanafunzi 53 tu ndio walichaguliwa kuingia katika chumba cha kufanyia mtihani kati ya wanafunzi 150 waliotakiwa kufanya mitihani.

“Mimi nina siku nne toka nikabidhiwe ofisi na Afisa Elimu wa Wilaya ya Kahama chini ya Afisa Elimu wake, Joseph Gwasa. Nilipokabidhiwa nilipewa maelekezo kuwa ni wanafunzi 53 ndio wanaopaswa kufanya mtihani wa kidato cha nne,” alisema Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Daniel Mtuli.

Mtuli alisema Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmanuel Maduhu, amesimamishwa kazi tangu Oktoba 3, mwaka huu, kwa sababu hizo hizo.

Alisema anasikitika kuona wanafunzi hao kupoteza muda wao kwa miaka minne na juzi kuambiwa kuwa hawawezi kufanya mitihani.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi hao walifanya maandamano kupinga kuzuiwa kufanya mitihani hiyo hadi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama.

No comments:

Post a Comment