Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, November 20, 2012

JK AZINDUA MKAKATI WA MASWALA YA SIASA, ULINZI NA USALAMA MJINI ARUSHA...!


VIONGOZI WA SADC wakiongozwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya mrisho kikwete katika picha pamoja

Muheshimiwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania akifafanua jambo katika mkutano wa SADC uliofanyika leo katika hotel ya ngorudoto

kikundi cha ngoma kikitumbuiza nje ya hotel ya ngorodoto
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho kikwete leo amezindua rasmi mkakati wa pili utakao shirikisha nchi za SADC utakao shughulikia maswala ya Siasa,Ulinzi pamoja na usalama .

Akizindua mkakati huo wa nchi za SADC leo katika hotel ya Ngurudoto iliopo nje kidogo ya jiji la Arusha alisema kuwa huu ni mkakati wa pili kuzinduliwa kwani mnamo mwaka 2004 mkakati wa kwanza wa ushughulikiao maswala ya siasa ,ulinzi na usalama katika nchi za SADC ulizinduliwa ila ulikuwa haujitoshelezi kutokana na kuwepo kwa mapungufu mengi .

Aidha alibainisha kuwa mara baada ya nchi hizo kubaini kuwa mkakati huo unamapungufu waliamua kufanya tasmini upya kuanzia mwaka 2009 na nchi zote zilitoa maoni upya na kurekebisha sehemu ambazo zina mapungufu ambapo alibainisha kuwa katika mkakati uliopita kuna mambo mengi yalikuwa hayajaingizwa ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na mtikisiko wa uchumi hivyo kurekebisha na mara baad aya kukamilika waliamu kuupitisha upya na jana (leo) ndo wamezindua rasmi na umeanza kufanya kazi rasmi.

Alisema kuwa shughuli moja wapo ambayo mkakati huu wa SIPO utaanza nao ni pamoja na kutatua matatizo yaliyopo DRC kongo ambapo alisema kuwa nchi hii inakabiliwa na mapigano makali yanayowahusisha wahasi wa kikundi cha M23 ambapo inapigana kwa mda mrefu na serekali ya kongo hivyo wao kama umoja wa nchi za SADC wameshauriana na viongozi kuona ni namna gani wanaweza kuzuia mapigano hayo yasiendelee na si hivyo tu bali wanaangalia ni jinsi gani wataweza kuwasaidia wananchi wanaoteseka nchini kongo.

Kikwete alisema kuwa katika kutatua tatizo hili nchi za SADC kwa kushirikiana na nchi za jumuiya ya maziwa makuu walishakaa kuongelea tatizo hili na walishakaa nchini Adis ababa kuongelea tatizo hili pamoja na kampala hii yote ni kutafuta jawabu la kutatua mgogoro wa nchini kongo katika eneo la Gomu .

Adha kwa upande wa mgogoro wa nchi ya Malawi na Tanzania kama utaweza kutatuliwa na SADC alisema kuwa mgogoro huo bado haujafikia katika kiwango cha dunia kwani mapaka sasa bado nchi yetu inamazungumzo na malawi na iwapo muhafaka hautapatikana basi watapeleka huko ila ni mapema sana kwa sasa kupeleka swala hilo wakati mazungumzo bado yanaendelea.

"hili swala la malawi bado alijaletwa katika nchi za sadc kwani bado tupo katika mazungumzo na naamini kabisa tutaelewana ila ikishindikana basi tutaleta huku ili muafaka upatikane maana kazi ya mkakati huu au chombo hichi cha tulichokizundua leo ndo kinashughulikia maswala hayo "alisem kikwete

Aimalizia kwa kusema kuwa anaimani kuwa mkakati huu uliozinduliwa leo utaweza kusaidia nchi hizi zilizopo katika jangwa la sahara kwa kiasi kikubwa katika kupunguza mambo mbalimbali kama uhalifu.

Katibu mkuu wa SADC Tomaz Augusto Salomao alisema kuwa mkakati huo utaweza kusaidi nchi hizi zilizopo katika jagwa la sahara katika mambo mengi yakiwemo ya kiuchumi ,utamaduni,siasa pamoja na ulinzi

No comments:

Post a Comment