Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, November 19, 2012

MAKOCHA WA SERENGETI BOYS WAONGELEA MCHEZO WA JANA: JULIO ALIA NA UMRI WA WACONGO, JACOB AHAIDI USHINDI MECHI YA MARUDIANO...!

KOCHA wa timu ya taifa ya vijana ya TANZANIA, SERENGETI BOYS, JACOB MICHILSEN amesema timu yake itacheza kufa na kupona katika mchezo wa marudiano dhidi ya CONGO BRAZAVILLE ili kuibuka na ushindi utakao iwezesha timu hiyo kupata tiketi
kushiriki fainali za Afrika kwa vijana zitakazo fanyika nchini MOROCCO mwezi MACHI mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya SERENGETI BOYS,na BRAZAVILLE jana,kocha MICHILSEN amesema katika maisha yake ya kucheza na kufundisha soka hajawahi kuona timu ngumu yenye umri chini ya miaka 17 kama CONGO BRAZAVILLE,lakini akawasifu vijana wake kwa kucheza vyema na kupata ushindi.
Wakati kocha mkuu wa kikosi hicho MICHILSEN akiyasema hayo msaidizi wake JAMHURI KIHWELO JULIO ameendelea kulalamikia umri mkubwa wa wachezaji wa CONGO BRAZAVILLE na tayari wamewasilisha lalamiko lao kwa kamati ya ufundi ya shirikisho la soka Tanzania TFF.
Bao pekee la SERENGETI BOYS lilifungwa na kiungo mkabaji MUDATHIR YAHYA ABBAS kwa mkwaju wa adhabu ndogo katika dakika ya 15 ya mchezo.
Mchezo wa marundiano kati ya SERENGETI BOYS na CONGO BRAZAVILLE utachezwa wiki mbili zijazo jijini LIBRAVILLE.

No comments:

Post a Comment