Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, November 19, 2012

MZEE WA MIAKA 75 MBARONI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI...!

MZEE wa miaka 75, mkazi wa kijiji cha Mahida anashikiliwa na polisi wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka nane. Habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro jana, Robert Boaz zilisema mzee huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Mkuu wilayani Rombo kwa uchunguzi zaidi.

“Yule mtoto amezoea kwenda kuchota maji kwa yule babu sasa kwa maelezo ya mtoto ni kwamba yule babu alimuingizia kijiti sio tendo la kubakwa lakini yote hayo ndio tunayachunguza,”alisema Boaz.

Hata hivyo taarifa nyingine zilizowakariri ndugu na majirani zilidai siku ya tukio hilo Alhamisi iliyopita, mwanafunzi huyo wa kike alikwenda kuchota maji akisindikizwa na mdogo wake wa kiume.

“Baada ya hilo tendo watoto walirudi nyumbani na ndio yule wa kiume akamwambia dada yake hebu mwambie babu (anayeishi naye) kuwa yule babu amekufanya nini,”alidai mmoja wa majirani.

Jirani huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alidai kuwa yule mtoto alieleza kila kitu na ndipo wazazi walipompeleka zahanati ya Mahida na baadaye Hospitali teule ya Huruma iliyopo Rombo.

Majirani hao akiwamo Padre mmoja wa Kanisa Katoliki, walidai baada ya madaktari katika hospitali hiyo ya Huruma kumfanyia uchunguzi, mtoto huyo alikutwa na Manii sehemu zake za siri.

Kutokana na hasira waliyokuwa nayo majirani hao, walihakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Holili lakini baada ya majirani kuchachamaa alihamishiwa kituo cha Mkuu.

Chanzo - Mwananchi

No comments:

Post a Comment