Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, November 22, 2012

UKISHAMPENDA, MUOE UMMILIKI LA SIVYO KAA TAYARI KUSALITIWA ...!

WIKI iliyopita utakumbuka nilianza kuzungumzia mbinu sahihi ya kukabiliana na tabia iliyoshimiri huko mtaani ya wapenzi kusalitiana.
Nikasema kama unatokea kumpenda mtu, kisha ukajiridhisha mtu huyo ni chaguo sahihi la moyo wako, unatakiwa kufanya jitihada za haraka kumuoa na kumuweka ndani.
Nilisema hivyo nikimaanisha kwamba, ukishamuoa unampunguzia yeye vishawishi mbalimbali vya wanaume.
Pia kwa kufanya hivyo utakuwa unajipa imani ya kwamba, wanaume wakware hawawezi kukutibulia licha ya kwamba wakiamua pia wanaweza kama huyo uliyemuoa atakuwa hajatulia.
Katika kuliweka sawa hilo, nikamtolea mfano kijana mmoja aliyebahatika kumpata msichana ambaye alimpenda sana lakini katika chelewachelwa ya kumuoa, akashindwa kumzuia na vishawishi na matokeo yake akajikuta anashea penzi na wanaume wengine.
Hebu msikilize huyu kijana kisha tuendelea, anasema: “Nilipobahatika kupata kazi nzuri niliapia kuoa mke mzuri. Katika pitapita yangu nikakutana na binti mmoja mzuri sana ambaye tulianzisha uhusiano.
“Binti huyo alionesha kunipenda sana, majina ya baby, sweetie, honey ndiyo aliyokuwa akiyatumia kuniita, hata siku moja hakuwahi kuniita jina langu.
“Kilichokuwa kinaniumiza kichwa ni kwamba, alikuwa na simu tatu na kila simu ilikuwa na line mbili. Sikujua ni za nini namba zote hizo na zaidi ya yote, alikuwa hapendi niguse simu zake.
“Siku moja tukiwa chumbani, alibanwa na kifua. Akazidiwa na kuwa na hali mbaya iliyonilazimu nimkimbize hospitalini. Siku hiyo ndiyo nilijua uozo wake wote.
“Yaani kila simu alikuwa akiwasiliana na wanaume wingine.”
Ushuhuda huu unatupa fundisho kubwa sana. Wasichana wengi wa mjini ni wazuri na wanayajua mapenzi kweli lakini wengi wao wametawaliwa na utapeli.
Unaweza kutokea kumpenda sana lakini kumbe yeye ana lake jambo, anakuchukulia kama wa kukuchuna tu na nyuma yako unachangia penzi na wenzako kibao.
Kikubwa ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na msichana yeyote na ukaona anafaa kuwa mkeo hata kama utabaini kuwa ni mapepe, fanya haraka umuoe.
Ukishamuoa angalau unaweza kuwa na imani kwamba hawezi kutoa ‘sukari’ yako kwa mtu mwingine licha ya kwamba, hata ukimuoa akiamua kukusaliti anaweza.
Kinachosaidia ukishamuoa ni kwamba, atatakiwa kufanya kazi ya ziada sana kukusaliti bila ya wewe kujua na hata akikusaliti haitakuwa kwa kiwango kikubwa kama akiwa mbali na wewe.
Tukae tukijua kwamba ulimwengu umeoza, kuna wanaume wapo tu na siku zote mitego yao ni kwa wake na wapenzi wa watu.
Lakini pia kuna wasichana ambao wana pepo wa ngono kiasi kwamba, mwanaume yeyote atakayemtokee ni saizi yake. Hali hii inamfanya kila aliye kwenye ulingo wa mapenzi kuwa makini ni mtu wake.
Chanzo:GPL

No comments:

Post a Comment