Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, December 12, 2012

HII NDIO VIDEO YA RAY C AKIWA IKULU NA RAIS KIKWETE, TAZAMA ALICHOKIONGEA RAY C NA MAMA YAKE...!

Siku mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila, maarufu kama RAY C, alipomtembela Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Desemba 10, 2012 Ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliyompatia wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni. Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake sasa imeimarika na kwamba muda si mrefu ujao atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake. Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray  C yamegharamiwa na Rais.

Hii hapa chini video ya Ray C na mama yake wakiwa ikulu na Raisi Mh. JK

No comments:

Post a Comment