Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, December 17, 2012

PICHA ZA BWANA HARUSI ALIYENUSURIKA KUFA KWA AJALI SIKU MOJA KABLA YA HARUSI YAKE...!


Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akiwa na mkewe Magreth Mtebe mara tu baada ya kufunga pingu za maisha jana katika kanisa la Agape jakaranda jijini mbeya. Bwana harusi anaonekana na majeraha baada ya kunusurika kifo katika ajali ya pikipiki na gari usiku wa kuamkia Jumapili ambayo alifunga ndoa.


Hii ndiyo ajali aliyopata bwana harusi emmanueli aligongwa na gari aina ya Toyota GX 100 Emmanuel yeye alikuwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia jumamosi mida ya saa sita nanusu usiku alikuwa anaenda kwenye mkesha kanisani ndiyo ajali hiyo ikatokea maeneo ya mafiati mbeya wengi wa mashuhuda hao walijua mwendesha pikipiki hiyo amekufa papo hapo 


Hii ndiyo hali halisi iliyotokea siku hiyo ya ajali mbeya yetu tulifika usiku huo eneo la tukio na kukuta tayari majeruhi wametolewa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa Mbeya ndipo jana tukaamua kufuatilia majeruhi hao na kukuta kuwa Emmanueli ameruhusiwa kwa muda akafunge ndoa kwani jana ilikuwa siku ya yeye kuoa ndipo tukaenda kufuatilia harusi hiyo katika kanisa la agape




Bwana harusi Emmanueli na mpambe wake Frank wakiingia kanisani

Hakika ni furaha hapa bwana harusi anamtambua mkewe kwa kumfunua shela kabla ya ndoa kufungwa


Sasa bana na bibi harusi wanaingia kanisani tayari kwa ibada ya ndoa


Mchungaji Emmanuel Mwasota toka E.A.G.T toka DSM ndiyo aliyofungisha ndoa hiyo


Hapa bwana harusi akimvisha mkewe pete huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea


Hapa wakipata mibaraka ya ndoa kutoka kwa wachungaji mbalimbali wa kanisa hilo la AGAPE


Sasa tu mwili mmoja kitakachotutenganisha ni kifo tu jina la bwana libarikiwe


Bwana harusi akipokea cheti cha ndoa toka kwa mchungaji Mwasota




Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa


Maharusi wakiwa na familia na wazazi wao


Sherehe fupi ya kuwapongeza maharusi ilifanyika katika bustani ya ccm jijini mbeya


Ndugu jamaa na marafiki walihudhuria sherehe hiyo ingawa maharusi hawakuweza fika kwenye sherehe hiyo kutokana hali yake haikuwa nzuri alihitaji kupumzika na kurejea tena hospitali kuendelea na matibabu


Picha na Gwasa wa Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment