Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, December 24, 2012

XMASS NDO HIYO HILI NI ANGALIZO KWA KINA DADA WAPENDA VYA BURE !!!!

Juzi Ijumaa ndiyo siku masham sham ya Sikukuu ya Xmass yalianza huku Moshi, Magari ya kifahari ya Wachaga yalianza kuingia ndani ya mji wa MOshi asubuhi, Mpaka kufika jioni mji ulikua umejaa sana.

Katikati ya mji wa moshi na Viunga vyake idadi kubwa ya kinadada ilionekana huku wakipita katika maduka mbalimbali kufanya manunuzi ya xmass. Ilipofika jioni hapo ndipo pilika pilika za kuelekea katika sehemu za starehe zilipoanza. {BAta Time}

Ndani ya Mji wa Moshi katika Uwanja wa Ushirika kulikua na Tamasha kubwa La muziki wa Dansi linalokwenda kwa jina la TUSKER CARNIVAL ambapo Bendi za muziki wa dansi Tanzania ambazo ni Twanga Pepeta International na Diamond Musica Original walikuwa wakitumbuiza.

Watu waliserebuka huku wakipata kinywaji Aina ya Tusker na nyama choma hakika ilikua shangwe sana. Ilipofika mnamo saa tisa na nusu Usiku Presenter aliyekua akiongoza Tamasha hilo Babi D'e Conscious alihitimisha Tamasha hilo hapo ndipo kilipoibuka kizaa zaa baada ya jamaa watatu kuanza kumgombania Binti mmoja anayesemekana ni mwanafunzi wa chuo cha Muccobs na kila mmoja akimtuhumu kanywa bia zake na nyama na anataka kuondoka nae.

                          Hapa ma baunsa wakimuokoa toka katikati ya watu.


Vurugu hizo zilizimwa na Walinzi wa Clouds Media baada ya kumuokoa dada huyo katikati ya kundi la watu akiwa anavuliwa nguo.

Hii ni changamoto kwa kina dada kwa msimu huu wa sikukuu, Kumbuka sikukuu ni kwa siku Moja tu ila Gharama ya maisha yako ni zaidi ya X mass.
                               HApa akisaidiwa kutoka nje ya Uwanja.


Yetu ndo hayo, Na wewe sema yakooooooooo....!

No comments:

Post a Comment