BARUA YA MASIKITIKO ALIYOIANDIKA PAPII KOCHA KWA MH. RAISI JK...!
MF/NA:
836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha) Gereza Kuu Ukonga S.L.P 9091 Dar es
Salaam Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania YAH: MAOMBI YA KUPEWA
MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA
HAKIMU MKAZI KISUTU. Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa
katika gereza kuu Ukonga. Kwa
heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya kiMUNGU
ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako
mitukufu muheshimiwa rais. Nakuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa
rais, kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya
kifungo cha maishagerezani,niliyohukumiwa
na mahakama tajwa hapo juu. Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana
mwenye umri mdogo, na ukweli kutoka moyoni sikufanya kosa hilo. Si mimi,
baba yangu Nguza wala ndugu yangu yeyote aliyefanya kitendo kile.
Lakini wenye mamlakawakatuona tuna hatia na kuamua kuteketeza kizazi
chetu gerezani. Natamani kiama ifike ili mwenyezi Mungu aweke wazi
ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia. Mpaka sasa natambua wazi hatima
pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh.
Rais Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako
ninaehitaji huruma yako wewe mzazi. Lakini pia sisi ni binadamu wenye
nafsi na miili kama wengine. Waliotumia mamlaka yao kutuweka gerezani
nao ni binadamu pia, wenye miili na nafsi. Ipo siku nafsi zetu zitapaswa
kutoa hesabu ya tuliyoyafanya hapa duniani. wakati huo miili yetu
tunayoitumia kunyanyasa wanyonge itakuwa imeoza mavumbini. Natumaini
kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu.
Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu. Mungu akubariki. Wako
mtiifu Mfungwa NO:836'04 JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA).
No comments:
Post a Comment