Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, February 9, 2013

KIGOMA ALL STAR KUUPAMBA USIKU WA VALENTINE'S DAY MOSHI

Wasanii wanaounda kundi la Kigoma all star wanatarajiwa kudondosha bonge la show katika ukumbi wa Aventure Africa Moshi, Akipiga Story na Chalii wa Moshi ambaye ni shushushu wa King Jofa, Mratibu wa Show hiyo aliyefahamika kwa jina Moja la Moses kutoka kampuni ya LEKATUTIGITE alisema Show hiyo itakuwa ya aina yake kwani wasanii wamejipanga vya kutosha kudondosha bonge la show itakayoacha historia kwa wapendanao wa pande za Moshi.


Pia Mratibu huyo aliendelea kusema zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wapendanao watakaopendeza watapatiwa zawadi ya Cheni ya silva na Hereni zake zenye thamani ya zaidi ya shilingi Laki nne na mwanaume atapatiwa brasslet ya silva yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nne kutoka Duka linaloongoza kwa uuzwaji wa Vito vya Thamani Kanda ya Kaskazini lililoko Boma Road mkabala na Bank ya Exim Bank mjini Moshi liitwalo Asms Peak Gemstone Dealers au Maarufu kama Sonara Sanaaaaaaa.

Akiwataja wasanii watakao upamba usiku huo ni pamoja na OMMY DIMPOZ, CHEGE, MAUNDA ZORO, BABA LEVO, ABDU KIBA, RECHO na PETER MSECHU. na pia burudani nyingine mbalimbali zitaendelea. Pia alitoa nafasi kwa wale wapendanao watakaopenda kuvalishana Pete za uchumba katika siku hiyo wawasiliane nasi mapema kupitia namba +255717636358 ili kuweza kutoa nafasi ya kufanya tendo hilo katika siku hii ya kihistoria duniani, Alimaliza kwa kusema hayo.

Lakini pia King Jofa hakuishia hapo tulipiga story na Omy Dimpoz alisema amejiandaa vya kutosha atahakikisha siku hiyo inatawaliwa na upendo zaidi kwani kuna suprise za kutosha kwa ajili ya wapendanao.

No comments:

Post a Comment