Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, March 25, 2013

WEMA SEPETU AMTENGANISHA KAJALA NA UKUTA WA GEREZA

Leo ilikua ni siku ya Huzuni sana kwa msanii wa Filamu Kajala MAsanja, na Pia ni siku ya Furaha na ya kihistoria katika maisha yake. Akiwa mbele ya Mahakama akisikiliza kwa Makini hakimu akisoma hukumu ya kesi inayomkabili, Hakimu akisoma vipengele vya sheria na mwisho alipomaliza kesi hiyo kwa kumuhukumu Kajala Masanja kwenda Jela miaka Nanea au kulipa faini ya Shilingi milioni kumi na tatu.

Hukumu hiyo ilikua ni mzigo kwa kajala iliyopelekea kutokwa na machozi akiwa kizimbani mbele ya wasanii wenzake wa bongo Muvi. Bila kuongea Chochote Icon wa Bongo Muvi Wema Isaack Sepetu alitoka eneo la Mahakama hiyo kimya kimya na kurudi baada ya muda akiwa na Fedha Taslim shilingi milioni Kumi na Tatu na kumtoa Kajala katika kifungo hicho. Bila kuamini kajala Hakuishiwa kutokwa na machozi huku akiwa haamini kama kweli Wema kamuokoa Kutoka katika kifungo.Kwa niaba ya KingJofa naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Wema Isaack Sepetu kwa Moyo aliouonyesha na pia kumpa Pole kajala kwa Mitihani ya maisha aliyopitia na sasa ni wakati wa kujipanga katika harakati za kulijenga taifa.

No comments:

Post a Comment