Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, April 11, 2013

WATATU WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA HANDENI...!

WATU watatu, wakiwamo waandishi wawili, Hussein Semdoe wa gazeti la Mwananchi na Hamis Bwanga wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo na Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Handeni, Mariam Hassan wamefariki papo hapo katika ajali ya kutisha iliyotokea leo Misima, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Marehemu Hussein Semdoe akiwa kazini. Picha hii ilipigwa mwishoni mwa wiki Kwamsisi wilayani Handeni mkoani Tanga

Watu hao walikuwa wakitoka Misima katika shughuli za kikazi na kusababisha vifo hivyo vilivyopokelewa kwa uchungu mkubwa na Watanzania wote, wakiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Afisa Elimu Shule za Sekondari wilayani humo, Simon Mdaki, alisema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya gari walilokuwa wanasafiria kupasuka tairi, hivyo dereva kulishindwa na kupinduka.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu
akiwa kwenye kazi za kijamii Kwedikabu, Kwamsisi

mwishoni mwa mwaka jana. Mwenye Kamera

ni marehemu Semdoe.
Alisema ajali hiyo ilikuwa nyuma ya gari ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Rweyemamu, aliyeambatana na watu hao ambao kwa sasa ni marehemu katika shughuli za kikazi Misima.

Ni majonzi makubwa yaliyotokea leo baada ya kuwapoteza Watanzania wenzetu, wakiwamo waandishi wawili na Afisa Uhamiaji ambao kwa pamoja tunasikitishwa kutokana na vifo vyao vilivyotokea katika ajali hii ya kutisha.

Mkuu wa Wilaya yeye hajaumia kwasababu gari lake lilikuwa la mbele, ingawa ni msafara wake kwa pamoja, hivyo tumeguswa na vifo hivi vilivyotokea katika wilaya yetu leo,” alisema.

Vifo vya waandishi hao ambao wana mchango mkubwa wilayani humo vitakuwa ni pigo kwa Watanzania wote, wakiwamo wananchi wa Handeni ambao kwa hakika mikono ya waandishi hao ilitumika vyema kuhabarisha umma kwenye vyombo vyao.

 
 
Chanzo: FatherKidevu

No comments:

Post a Comment