Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, May 7, 2013

MUENDESHA BODABODA AHUSISHWA NA ULIPUAJI WA KANISA ARUSHA...,

Watu waliojeruhiwa katika tukio la kulipuliwa kwa bomu katika kanisa la katholiki parokia mpya ya olasiti jijini arusha wamezidi kupoteza maisha kutoka watu wawili na kufikia watatu huku baadhi yao wakiendelea vizuri na matibabu.
Hayo yamezungumzwa na Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa arusha maunt meru Dkt Frida Mokiti na kuongeza kuwa mpaka sasa wamebaki majeruhi 31 toka majeruhi 66 waliowapokea katika hospitali hiyo.
Sanajari na hilo pia Dkt mokiti amsema kuwa kati ya majeruhi hao 31 baadhi yao hali zao ni mbaya ingawa wengi wao wameruhusiwa kurudi nyumbani mara baada ya hali zao kuwa nzuri.
Hata hivyo ameeleza kuwa madktari wanaendelea na huduma kama kawaida kuhakikisha wananusuru maisha ya majeruhi hao na kuwaomba wakazi wa jiji hilo pamoja na watanzania kwaujumla kuendelea kuwaombea kwa mungu ili majeruhi hao ili waweze kupata uzima.


Mmoja wa majeruhi wa Mlipuko wa Bomu katika katoliki parokia mpya ya Olasiti la jijini Arusha  akipata matibabu.

Sambamba na hilo pia kamishna msaidizi wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha kamanda Liberatus Sabas ameeleza kuwa mpaka sasa Jeshi la polisi mkoani hapo linawashikilia watu kumi [10] kuhusika na tikio hilo huku kati yao watu wanne wakiwa ni kutoka nchini saudiarabia.

Muonekano wa kanisa la Olasiti kwa nje baada ya Mlipuko wa Bomu kutokea.

Aidha kamanda Sabas ameeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa mara baada ya maojiano yaliyokuwa yakifanyika baina ya mtuhimiwa wa kwanza alie kamatwa na jeshi la polisi kijana Vikta [20] mkazi wa olasiti dereva pikipiki [toyo] hatimae kutaja watuhumiwa wenzake waliohusika katika tukio hilo.
Hata hivyo kamanda Sabas amesema kuwa kamwe jeshi la polisi mkoani hapo pamoja na wanajeshi nchini kote hawatalifumbaia macho suala hilo ikiwa ni sambamba na matukio mengine ya kikatili ya namna hiyo mpaka pale watakapo hakikisha amani na utulivu inatawala ncnhini kama ilivyo kuwa awali.

No comments:

Post a Comment