Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, June 10, 2013

KIDUMU AFUNGUKA KUHUSIANA NA SHINDANO LA MISS KILIMANJARO


            WAREMBO WANAOWANIA TAJI LA MISS TANZANIA KILIMANJARO 2013

 Ikiwa Tarehe 15 mwezi wa sita siku ya Jumamosi ndiyo siku ambayo Mkoa Kilimanjaro utamtoa Mrembo katika shindano linalotambulika kimataifa katika masuala ya urembo linalotambulika kama Redd’s Miss Tanzania Kilimanjaro 2013. Homa ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro na Miji yake inazidi kukuabaada ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Rick Plan & Co. Ltd Jackline Chuwa kupitia kampuni yake ambayo ina dhamana ya kusimamiana kuandaa mashindano hayo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro Kutangaza Mwanamuziki atakayetumbuiza katika Usiku huo wa Urembo. Baada ya Jina la Mwanamuziki wa kimataifa kutoka Rwanda anayetambulika kwa Jina la KIDUMU kutajwa kuwa moja wa wanamuziki watakaodondosha burudani katika ukumbi wa LALIGA CARNIVAL timu nzima ya Kingjofa iliamua kumtafuta Kidumu na ku zungumza nae kuhusiana na Siku hiyo.  


            KIDUMU AKIZUNGUMZA NA KINGJOFA

 KINGJOFA. Ngrii ngriii….! KIDUMU: Hallow..!
 KINGJOFA: Ndio naongea na Kidumu
 KIDUMU: Yes ndio mimi, Nani mwenzangu?
 KINGJOFA: Mimi ni shabiki wako nipo Moshi mkoani Kilimanjaro KIDUMU: Oh sawasawa habari KINGJOFA: Nzuri tu, Nasikia wewe utakuwa Moshi Tarehe 15 mwezi huu wa sita ni kweli?
 KIDUMU: Ndiyo, Ni kweli na sitokuwa peke yangu nitakua na Bendi yangu yote kutoka huku Rwanda. KINGJOFA: Vipi mbona umekua kimya sana.
 KIDUMU: Nilikua katika Ziara ya kimuziki huko Ulaya na Show Hiyo ya Miss Kilimanjaro ndiyo itakua show ya kwanza Afrika baada ya kumaliza 
Ziara yangu Ulaya.
 KINGJOFA: Unatuahidi nini sasa sisi mashabiki wako?
 KIDUMU:Siku hiyo nitafanya kitu ambacho kitakua ni historia kwa nchi za Afrika Mashariki, Si unajua mimi napiga vyombo na naimba Live sasa Wakazi wa huko wakae Tayari kumuona Kidumu wa Kimataifa. KINGJOFA: Sawa Pia mimi nitakuwepo nitakaa viti vya mbele ili nikuone vizuri 
KIDUMU: Sawasawa, Usikose Show hii ya Miss Kilimanjaro hiyo tarehe 15 pale Laliga Carnival.

 Hayo ndiyo mazungumzo ya Kingjofa na Kidumu aliyekua akiongea moja kwa moja kutoka Rwanda wakizungumzia Usiku wa Shindano la Redd’s Miss Tanzania Kilimanjaro 2013 ambalo linatarajiwa kufanyika Tarehe 15 mwezi huu wa sita katika ukumbi wa Laliga Carnival. Shindano hili likiwa limedhaminiwa na Redd’s Original, Bonite Bottlers Ltd, Panone and Company Ltd, K.C.K Traders, Qwine Hotel, Africa sana Holili, Hugos Hotel, Kingjofa blog, Michuzi Blog.

1 comment:

  1. Thank you for current and updated informations

    ReplyDelete