Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, June 13, 2013

MAMBO MATANO MUHIMU KUHUSU KING GK..!

Mambo Matano Muhimu kuhusu King GK...!
Baada ya ukimya wa zaidi ya miaka mitano ambao pia ulimfanya asitake kuongea kwenye chombo chochote cha habari, amekua akikataa interview kwa kipindi chote, hatimae Kamanda mkuu wa kikosi cha East Coast, King GK ametoa ya moyoni.

Kwenye backstage ya KTMA 2013 kwenye Exclusive interview, GK amezungumza mambo matano makubwa kuhusu yeye na muziki wake.

1. Baada ya ukimya wa zaidi ya miaka mitano, single yake mpya ya kurudi kwenye game rasmi inatoka kwenye kipindi kisichozidi mwezi mmoja kutoka sasa.

2. Uhusiano wake na Mwana FA na Ay uko poa kwa sasa.

3. Mpaka sasa amesharekodi nyimbo mpya zisizopungua sita zikiwemo kolabo ambapo Ay na Mwana FA wameshirikishwa.

4. East Coast bado ipo na itazidi kuwepo.

5. Hawezi kutaja tarehe rasmi ya kurudi kwa sasa kwa sababu anataka iwe surprise.

Kauli kama hizo kutoka kwa GK ni good news kwa kila shabiki anaemfahamu baada ya miaka mingi ya ukimya wa East Coast, ambayo ilianza kuwa kimya baada ya mastaa kadhaa kuanza kujiondoa kutokana na kutofautiana wakiwemo Ay na FA.

GK alikua mmoja wa wageni walioshiriki kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali wa KTMA 2013.


YOU MIGHT ALSO LIKE THIS

No comments:

Post a Comment