Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, June 7, 2013

Mbunge wa Mbarali ahukumiwa kwenda Jela…!

MBUNGE wa Mbarali, Modestus Kilufi (CCM) amehukumiwa kifungo cha miezi 10 baada ya kupatikana na hatia ya kutishia kuua, Mbunge huyo (51) alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Oktoba 10 akidaiwa kutishia kumuua Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa, Mbarali, Jordan Masweve.
Kabla ya kusoma hukumu hiyo leo Mbunge aliomba Mahakama impunguzie adhabu, kwani ana watoto watano kati yao wawili wanasoma Chuo Kikuu na wananchi wanamtegemea kuwasilisha matatizo yao bungeni.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Michael Mteite, alisema ameridhika na ushahidi wa upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wa Serikali, Epimack Mabrouk na Griffin Mwakapeje, pia mawakili wa upande wa mashitaka walimwomba Hakimu Mteite kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.“Kutokana na maelezo hayo na ushahidi ulioletwa mahakamani, ninakuhukumu kifungo cha miezi 10 jela” alisema Hakimu Mteite.
Mbunge akihojiwa katika chumba cha mahakama alisema unajuwa sikuhizi haki inatendeka pale tu iwapo mwanaccm ametiwa hatiani, lakini kama ni mpinzania ametiwa hatiani utasikia ooh kaonewa au hii ni hukumu kutoka ikulu, hata hivyo alisema atakata rufaa katika hukumu hiyo.
.Modestus Kilufi


source:jamiiforums (21)
YOU MIGHT ALSO LIKE THIS

No comments:

Post a Comment