Rais
mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa hospitalini kwa siku
ya nne ambako anapokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu. Duru kutoka kwa
ofisi ya rais Jacob Zuma, zinasema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94,
yuko katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa.Jamaa zake pamoja na
aliyekuwa mkewe Winnie Madikizela-Mandela, walimtembelea hospitalini
Jumatatu Mwanawe Mandela Zenani (Mandela-Dlamini), pia alirejea kutoka
nchini Argentina, ambako yeye ni balozi.Serikali imekuwa ikisema kuwa
hali ya Mandle inatia wasiwasi ingawa madaktari wameweza kuidhibiti.
Amekuwa katika chumba ya wagonjwa mahututi tangu kulazwa hospitalini
Jumamosi kwa mara ya tatu mwaka huu.Mwezi Disemba , bwana Mandela
alilazwa hospitalini kwa siku 18 baada ya kupata maradhi ya mapafu,
Kumekuwa na taarifa za simanzi kwa mara ya kwanza huku familia yake
ikikusanyika kando yake, baadhi ya watu wakisema kuwa ni muda wamwache
Mandela aende zake.Bwana Mandela, mwenye
umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni
mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu. Kwa mujibu wa duru za urais,
Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa
tena na ugonjwa wa mapafu. Msemaji wa serikali Mac Maharaj amesema kuwa
maafisa katika hospitali wanataka kudhibiti idadi ya watu wanaozuru
hospitali hiyo ili wampunguzie bwana Mandela usumbufu. Alilazwa
hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.Kwa
mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito
wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu
anapougua. Watu wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi,
kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.Mkewe
Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi
ili kuwa kando ya mumewe. Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya
mwaka 1994 hadi 1999.
No comments:
Post a Comment