Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, June 6, 2013

UPDATES KUTOKA MOROGORO: WAKAZI WAANZA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU MANGWEA..!

Mama Mzazi wa Mangwea, Denisia Mangwea akiwa nyumbani kwake kabla ya safari kuelekea Uwanja wa Jamhuri.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiwasili nyumbani kwa Mama mzazi wa Mangwea.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera asubuhi hii amefika nyumbani kwa Mama Mangwea eneo la Kihonda Mazimbu Road na kumpa pole kwa niaba ya wakazi wote wa mkoa wa Morogoro. Baada ya kutoa pole, Mhe. Bendera aliongoza umati wa watu kutoka Kihonda kuelekea Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli za kuaga mwili wa Albert Mangwea aliyefariki dunia Mei 28 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Mangwea anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kihonda nje ya Kanisa la Mtakatifu Monica jirani kabisa na alipozikwa baba yake mzazi Mzee Keneth Mangwea.

Wakazi wa mji wa morogoro waanza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Albert Mangwea kabla ya kumpeleka katika Nyumba yake ya Milele. Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala Pema.

Baadhi ya wasanii na wananchi waliohudhulia uwanjani wakati wa kuaga mwili wa marehemu albert mangwea uwanja wa jamhuri morogoro. 

Watu wakiaga mwili wa Marehemu albert mangwea uwanja wa Jamhuri morogoro.

No comments:

Post a Comment