Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, July 14, 2013

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YATOKEA MAENEO YA KAWAWA ROAD MJINI MOSHI...!


Hivi ni baadhi ya vyuma vya gari lililopata ajali maeneo ya barabara ya kawawa (kawawa road)

 Hili ni basi la metro coach baada ya kupata ajali.
  Haya ni mabaki ya basi la metro coach baada ya kupata ajali mbaya.
 LEO usiku majira ya saa moja ajali mbaya na yakusikitisha imetokea eneo la barabara ya kawawa (kawawa road) iliyosababishwa na gari aina ya fuso iliyokua ikitokea maeneo ya moshi mjini na kuelekea upande wa njia panda ambapo dereva alipokua kwenye spidi kali na kutaka kulipita gari lingine bila kuangalia kama kuna gari lingine mbele alijikuta akisababisha ajali mbaya baada ya kukutana uso kwa uso na basi la abiria la Metro coach linalofanya safari zake Dar - Arusha.
Ambapo basi hilo limepata ajali hiyo mbaya likiwa limebakiza kilometa chache kufika Moshi Mjini. Taarifa za awali ni kwamba mtu mmoja amefariki papo hapo ambaye ni dereva wa basi la Metro coach na kuna majeruhi wengine zaidi ya kumi waliojeruhiwa vibaya katika ajali hiyo. Wapo majeruhi ambao wapo kwenye hali mabya sana ila tayari wasamaria wema wameshapatia msaada wa kuwapeleka hospitali kwa ajili ya matibabu. 
Habari zaidi kuhusu ajali hii endelea kutembelea www.kingjofa.blogspot.com

No comments:

Post a Comment