Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, July 5, 2013

HATIMAYE MKOA WA MBEYA WAGAWANYWA NA KUWA MIKOA MIWILI


  
MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKIFUNGUA MKUTANO WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA(RCC)  JIJINI MBEYA

 
KATIBU TAWALA WA MKOA MARIAM MUTUNGUJA AKISOMA TAARIFA YA MKUTANO 
 
  
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PHILIPO MULUGO AKICHANGIA JAMBO WAKATI WA KIKAO HICHO


MBUNGE WA MBOZI MASHARIKI NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MBEYA GODFREY ZAMBI AKICHANGIA JAMBO KATIKA KIKAO HICHO


 MKUU WA WILAYA WA MBEYA  DR. NORMAN SIGARA  AKIZUNGUMZA  KATIKA MKUTANO HUO 


 MBUNGE WA VITI MAALUMU(CCM) MKOA WA MBEYA  DR. MARY  MWANJELWA  AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO.


MEYA WA JIJI MBEYA ATANAS kAPUNGA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO

  
 MKUU WA  WILAYA YA  RUNGWE  CRISPIN MEELA AKIZUNGUMZA JAMBO 


WAJUMBE  WAKIWA WANAFUATILIA MKUTANO HUO 

 
Songwe ndilo jina lililopendekezwa kuwa la Mkoa Mpya utakaogawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya ambao utakuwa na Wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba ambapo Makao makuu ya Mkoa huo utakuwa Mkwajuni Wilayani Chunya.

Mkoa wa zamani Mkoa wa Mbeya utabaki na Wilaya za Rungwe, Mbarali, Mbeya na Kyela ambapo Makao makuu yatabaki pale pale Jijini Mbeya.

Kupatikana kwa jina hilo na mwafaka huo kumetokana na Mkutano wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa uliofanyika leo katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.

Jina la Mkoa huo Mpya limetokana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Songwe na Mto mkubwa unaoitwa Songwe ambao unapita katika Wilaya zote zinazounda Mkoa huo mpya.

Hata hivyo kuhalalishwa kwa jina na Mkoa huo unategemewa na Mamuzi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kupelekewa mapendekezo hayo ya RCC.

No comments:

Post a Comment