Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, July 9, 2013

Kuhusiana Na Agnes 'Masogange' Kukamatwa Na Dawa Za Kulevya Afrika Kusini, SomaHhapa


Kufuatia taarifa hii kutoka katika magazeti ya leo;

"Wanawake wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.


Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini".

Mwanadada Agnes Masogange kwa sehemu kubwa anahisiwa kuwa ndiye mhusika ambaye yupo kizuizini huko Afrika kusini kwa kesi hii, bado tunaendelea kufuatilia kwa makini ili kupata uthibitisho wa taarifa hizi na kama ni kweli Mtuhumiwa aliye kamatwa ni Agnes Jerald... maarufu zaidi kama Agnes Masogange.
 
Aina yake ya maisha ya hali ya juu bila jamii kujua wazi ni kitu gani anachokifanya kujipatia kipato, pamoja na binti huyu kuwa na Safari nyingi za Afrika Kusini ni moja ya sababu ambazo zinaongezea nguvu swala la kuwepo kwa ukweli katika taarifa hizi kwa mujibu wa wadau.
Unaweza kutuambia hapa maoni yako ni nini kuhusiana na issue hii nzima wakati huu ambapo harakati za ufuatiliaji ili kupata ni upi hasa ukweli wa taarifa hii zinaendelea.
Ripoti kutoka SA;

No comments:

Post a Comment