Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 11, 2013

MSIBA: Joyce kiria wa East Africa Television amefiwa na baba yake mzazi.


Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live Joyce Kiria amepatwa na msiba baada ya baba yake mzazi aliyefariki jana mkoani Tanga alipokuwa akiishi.
Katika taarifa tulizozipata kupitia ukurasa wa facebook wa kituo cha television cha EATV Joyce aliandika
“Leo ni siku nyingine ya historia kwenye maisha yangu baada ya baba yangu Michael Francis Iwambo Kiria wa Kibosho Dakau Nganyeni kufariki huko mkoani Tanga ambako alikuwa akiishi. Kesho (leo) ni safari ya kuelekea Moshi kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Im speechless... R.I.P MY DAD"
Joyce kiria ni mmoja wa wadau wakubwa sana wa filamu nchini, na ni mtu aliyetoa na mchango wa pekee katika kukuza tasnia ya filamu nchini kupitia kipindi chake cha bongo movies kabla hajaanza kutangaza kipindi cha wanawake live kupitia kituo hicho hicho cha EATV
MSIBA: Joyce kiria wa East Africa Television amefiwa na baba yake mzazi.
Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.

No comments:

Post a Comment