Babi akiwa kwenye Fiesta Road show 2012.
Babi akisherehesha katika mahafali ya Green Bird College iliyopo katika Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Babi akisherehesha Miss Moshi 2013.
Babi akiwa na Luiza Nyoni Mbutu wa Twanga pepeta kabla ya Show ya Tigo Bonanza Dodoma
Babi akiwa na Masanja Mkandamizaji wakisherehesha kwenye Miss kilimanjaro Launch part
Babi akiwa anafanya Panone Road show.
Babi akiwa katika studio za 96.5 Kibo fm Radio, akifanya kipindi.
Babi akiwa na warembo wa Miss kilimanjaro 2013 wakifanya Tourkatika makampuni mbalimbali yaliyotoa udhamini.
Babi akiwa kwenye Tigo Bonanza katika viwanja vya CCP mjini Moshi.
Babi akiwa kwenye Tusker Carnival Uwanja wa Ushirika.
Babi akiwa kwenye Vodacom Road show.
CASSIM ni mtoto kwanza kati ya watoto watatu wa
Familia ya Mr. & Mrs. Shaaban Mwinyi. Mwaka 2001 alijiunga na Shule
ya Sekondari Mawenzi iliyopo mjini Moshi. Baadae alijiunga na ufundi
katika gereji ya Sawaya iliyopo majengo mjini Moshi kwa sasa inafahamika
kama Kilimanjaro.
Baada ya hapo alipata mafunzo ya Facilitation skills
na kufanya kazi katika shirika la White Orange Youth kwa muda wa mwaka
mmoja na mwaka 2006 alipata kazi katika shirika lingine liitwalo Child
Health and Social Ecology aliajiriwa kwa mkataba wa mwaka mmoja kama
Assistant Facilitator.
Baada ya mkataba kuisha akapata nafasi ya kufanya
katika mradi wa Family Health International katika mradi wa Ishi
Campaign akiwa kama Youth Advisory Group Wakati akifanya kazi hiyo
aliweza kufanya kazi ya muda katika shirika la Kikristo la YMCA kama
Facilitator katika kitengo cha Education.
Mwaka 2008 alienda Nairobi katika Mafunzo ya East Africa Leadership and
Citizenship Program akiwakilisha Tanzania, anakiri kuwa mafunzo
aliyoyapata yalimfanya ajitambue kuwa ana uwezo binafsi na anaweza
kufanya kitu chochote. Maana alifundishwa kujiamini na Kufanya kitu na
sio kujaribu. Baada ya kumaliza mafunzo hayo mjini Nairobi alirudi Moshi
na wazo la kutengeneza Film yenye kiwango cha juu ambapo kwa kipindi
hicho film za Tanzania zilikua za kiwango cha chini sana ilibidi
nitafute watu ambao wanaweza fanya kazi ndipo akawapata jamaa ambao
waliweza kukubali wazo lake na kujitolea muda wao kuhakikisha kuwa
Cassim anafikia lengo lake.
Jamaa hao ni Julius Masaoe ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Phijema video
Production, Benson Jackson ambaye ni Muandishi wa habari, Hamis Kitunga
huyu ni kijana Mjasiriamali na Thomas Munuo huyu ni Director wa
Viafrica. Hapo ndipo ikazaliwa Kampuni ya Africa Film.
Baadae aliweza kuandika films nyingi za Kibongo na kuziuza film kama
“Zawadi ya Birthday” ya JB, “My Heart” na nyingine nyingi. Pia Cassim
anafanya kazi kwenye kituo cha radio kinachoitwa “Radio Kibo Fm” iliyopo
mjini Moshi.
Licha ya kufanya kazi kwenye kituo cha radio pia ni
presenter kwenye matamasha mbalimbali na kati ya matamasha ambayo amewai
kuyafanya ni kama Fiesta, Promotion mbalimbali, Matamasha ya Vodacom,
Tigo, Airtel, event za TBL na hata za mashirika ya kijamii. NGO's.
Mashindano ya Miss Kilimanjaro, Miss Utalii, Miss Simanjiro. Road Shows
nyingi sana na mengine mengi sana.
Mwishoni mwa mwezi wa nane atakua pale Tabora katika uwanja wa Ally
Hasan Mwinyi kutakua na Bonge la Event litakalowashirikisha wasanii wa
Bongo Movies na wasanii wa Muziki wa Bongo flavor. Pia nafundisha watu
wanaopenda kuwa ma Presenter chini ya kampuni ya Somjo Dj's.
Nikapata
fursa ya kumuuliza tofauti kati ya Presenter na MC? “Tofauti ya
Presenter na Mc kwanza MC lazima uvae suti au suruali ya kitambaa halafu
uchomekee ila Presenter unavaa hata kaptula ila swaga ndio zinahusika
MC anafanya kitu uniform yaani MC wanafanya vitu vya kufanana kuanzia
mavazi mpaka mpangilio wa matukio kitu ambacho kwa Presenter huwezi
kukiona kabisa.
Mfano ratiba za ma MC huwa hivi Kufungua kwa sala Utambulisho Kufungua
shampeni, kukata Keki, kula Chakula, kutoa Zawadi, Nasaha kutoka kwa
wazazi na Kufungua mziki yaani hiyo ndo ratiba yao labda vipengele
vipishane cha juu kiwe chini cha chini kiwe juu ila hicho cha kwanza
lazima kianze.
Presenter huwa hawafanani swaga yani ukimkuta leo hapa
kesho ni mwingine anaweza anza kwa kudondosha show au story ya
kufurahisha. Yaani yeye anapewa anaambiwa kinachotakiwa kufanyika tu ila
Presenter anafanya mpangilio wa shuhuli nzima. So mimi mtu akiniita MC
sipendi kabisa japo njaa ikizidi nakula hata mifupa yaani nafanya hata u
MC.
Mfano Mahafali ya Green bird School na Green Bird College
nafanyaga mimi ila huwa siwi MC nakuwa Presenter japo wananiita Mc ila
wananiambiaga sifanani na ma MC huwa nacheka sana wanaposema hivyo najua
hawajui kama Mimi ni zaidi ya MC.
Kwa upande wa Changamoto ambazo anakutana nazo ni nyingi sana kwanza ni
kwenye malipo malipo si makubwa sana kulingana na kazi na pia Vishawishi
ukiwa si mgumu unaweza ukafa na ngoma (UKIMWI) maana watoto wazuri
wanataka ku date na wewe sababu wanaona kuwa Presenter ni mtu maarufu
na kila wasichana wengi wanapenda kuwa na watu maarufu.
Wakati mwingine anakua barabarani akitangaza tamasha mfano la wanamiziki
mtu anakuja anaomba tiketi ya free kutoka kwako bila kufikiri unafanya
kazi ya watu na hauhusiki na ukimwambia ukweli anakwambia unaringa.
Mafanikio aliyoyapata ni mengi kama kuwasomesha wadogo zake wawili,
elimu ya sekondary, ameweza kujisomesha mwenyewe Uandishi wa Habari,
anaishi kwake na ana maisha mazuri pina ana network kubwa sana ya kazi
na makampuni mbalimbali na hata watu binafsi wanamuamini.
Kwa sasa anamiliki
Movie Lab ambayo inaitwa “The Music Lab” ipo meneo ya Majengo mjini
Moshi ambapo unaweza kupata Movies za aina zote Latest na Music ya aina
zote kuna Mashine ya kuandika tishet na Jersey, Vikombe na hata ku print
picha katika nguo. stiker, vifaa vya simu na muda si mrefu kutapatikana
simu za bei rahisi kuanzia elfu kumi na kuendelea juu.
Matarajio yake ya baadae ni kuwa na kampuni ya Marketing and Promotion
na kuwa Presenter mwenye heshima kubwa sana Tanzania na nje ya Tanzania.
Ukitaka kumpata Cassim kwa ajili ya kazi piga simu +255717636358 utaweza
kumuuliza chochote na atakupa majibu ya uhakika.
No comments:
Post a Comment