Leo
 akiwa anawahutubia wakazi wa mabibo-Sahara kwa mara ya kwanza toka 
atoke jela huko gereza la uyui- Tabora katika mkutano ambao mgeni rasmi 
alikua Mh. John Mnyika mbunge wa jimbo la Ubungo, Henry Kilewo aliwaliza baadhi ya wananchi waliofika katika 
mkutano huo. Hii kutokana na kuguswa na hotuba ya kamanda huyo wa chadema ambayo 
ilikua inaudhunisha kutokana na simulizi ya namna alivyokamatwa na kupelekwa jela na pia aliweza kutoa ushuhuda wa jinsi watu wengi wanyonge na maskini waliofungwa pasipo na hatia.
Kutoka kwenye chanzo cha habari hii alikiri kuwa kweli simulizi ile inasikitisha lakini bado alisisitiza kwa kusema "Hakuna 
dhambi kubwa hapa duniani kama uoga'" na  watatupiga kwa mabomu na 
watatu ua kwa risasi lakini na wao watakufa kwa presha ya dhambi.
No comments:
Post a Comment