Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 11, 2013

ANGALIA PICHA ZA AJALI ILIYOTOKEA ARUSHA ABIRIA ZAIDI YA AROBAINI WANUSURIKA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JIJINI ARUSHA


Hii ndio coaster iliyopata ajali ambayo baada ya ajali ilihama barabarani na kuelekea vichakani.

Huu ni upande wa mbele wa garri aina ya Suzuki Escudo ambao unaonekana kuumia sana, na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakishangaa jinsi ambavyo gari hiyo imeharibika.

 Huu ndio upande wa mbele wa coaster iliyopata ajali na abiria wote kutoka wakiwa wazima wa afya.

        ARUSHA jana usiku majira ya saa moja ilitokea ajali mbaya iliyohusisha gari  aina ya Escudo yenye nambari za usajili T600 AUC na Coaster yenye nambari za usajili T598 BNS. Ajali hiyo iliyotokea eneo la Makumira, wilayani Arumeru, jijini Arusha. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema chanzo cha ajali hiyo wamesema kuwa ni gari aina ya coaster iliyokua ikitokea jijini Arusha na ilipofika eneo la makumira ilitaka kupita gari iliyokuwa mbele lakini kabla gari hiyo haijamaliza kuipita gari hiyo, kumbe mbele kulikua kuna gari aina ya Escudo iliyokua ikitokea Moshi kuelekea Arusha ndipo zilipokutana uso kwa uso na kusababisha ajali mbaya.   

Katika ajali hiyo hakuna hata mtu mmoja aliyefariki ila dereva wa gari aina ya Escudo aliyefahamika kwa jina moja la Hussein maarufu kama Baunsa ndie aliyeumia sehemu za miguuni na kichwani lakini wasamaria wema waliweza kumtoa katika eneo la ajali na kumuwahisha hospitali. 

#teamKINGJOFA

No comments:

Post a Comment