Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa
katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika
ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini.
Milio hiyo ilidumu kwa dakika tatu na kufuatiwa
na moshi mkubwa juu ya jengo hilo. Hakuna taarifa kamili kuhusu
kilichosababisha moshi huo.
Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka
nyara raia ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo
wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa
Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.
Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Aidha wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.
Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na milipuko imesikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.
Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.

Rais Kenyatta amesema kuwa jeshi linajitahidi kuhakikisha kuwa linakabiliana vilivyo na wanamgambo hao.
Helikopta za polisi zinazunguka juu ya jengo
hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika doria. Vikosi vya usalama
vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru waathiriwa wakati hali
ikiwa ni ya ati ati katika eneo la shambulizi.
Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti
jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa katika
kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.
Ripoti zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika
shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa. Baadhi
wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni
majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al shabaab
waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya Jumamosi.
Kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo
kutokana na hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini Somalia ili
kukabiliana na wapiganaji hao.
Source: TheChoice Blog
No comments:
Post a Comment