Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 28, 2013

CCM MANISPAA YA MOSHI YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAISI JAKAYA KIKWETE

 
 Muonekano wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
MOSHI Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Moshi kimeanza kutekeleza agizo la mwenyekiti wa taifa wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete la kutoa mafunzo kwa watendaji wake kuanzia ngazi za matawi na kata ilikutambua wajibu wao katika kuitumikia pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika manispaa hiyo kwa niaba ya katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kazidi katibu wa CCM wa Manispaa ya Moshi Aluu Segamba alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa watendaji wa chama hicho pamoja na jumuiya zake.

Segamba ameyataja mambo yatakayofundishwa nipamoja  mada mbalimbali zikiwemo uandaaji wa vikao,utawala bora, uandaaji wa mikutano ya hadhara pamoja na muongozo wa utunzaji wa fedha na mali za Chama Cha Mapinduzi.

Nao baadhi ya watendaji waliyoshiriki katika mafunzo hayo wamesema kuwa yamewajengea ujasiri mkubwa hivyo wataweza kufanya kazi zao kwa kujiamini zaidi kwakuwa wametambua nini wajibu wao katika kukitumikia chama na jamii kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment