Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 31, 2013

Kila Kilometa Nitakayokimbia Mtoto Atakuwa Darasani

Hii ni kauli mbiu ya John Kessy kwa lengo la kuchangia elimu ya msingi kwa kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathoni zitakazofanyika mwakani tarehe 2 March 2014 mkoani Kilimanjaro.

Msaada huu umelenga watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kupata haki yao ya elimu. John amekuwa akishiriki mbio za nusu marathoni kwa miaka mingi tangu zihasisiwe mbio hizo za Kilimanjaro marathon mjini Moshi ila kwa sasa itakuwa ni mara ya kwanza kwa John kushiriki mbio ndefu (full marathon) ili kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Wewe kama rafiki, ndugu na mpenda maendeleo unaombwa mchango wa fedha kwa ajili ya karo, sare na ada ya chakula. Na lengo ni kukusanya fedha zitakazowatosheleza mahitaji ya watoto 42. Watoto hawa wanapatikana katika shule za msingi zifuatazo: Majengo, Njoro, Mzalendo, Mandela, Jitegemee, Msufini na Katanini.

Endapo utahitaji maelezo zaidi kuhusiana na mpango huu tafadhali usisite kuwasiliana na John Kessy.
Shukrani za pekee zinatangulizwa kwa kila mchango utakaotolewa.

Pia unakaribishwa kupata maelezo zaidi kwenye blog hii http://johnkessy.wix.com/john-kessy

No comments:

Post a Comment