Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 22, 2013

HII NDIO TAARIFA RASMI KUHUSU KUWAVUA UONGOZI ZITTO KABWE, Dr. KITILA NA SAMSON.

Taarifa rasimi ya CHADEMA kuhusu kuwavua uongozi Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba. Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewavua Uongozi Viongozi wake watatu baada ya Kugundua waraka wa Siri uliowahusisha na mpango wa kukipasua Chama vipande vipande. Viongozi waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini. Akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari Mh. Tundu Lissu amesema katika Waraka huo kulikuwa na mtu anayejulikana kama MM ambaye ni Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni Mwigamba na M2 hajajulikana ambaye ni mtumishi wa makao
makuu ya Chadema. Mh Lissu amesema Dr Kitila Mkumbo alikana kabisa kumfahamu M2. Mh Tundu Lissu anasema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA. Mh.Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu

No comments:

Post a Comment