Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, November 21, 2013

TV YETU LEO:- RAIS J.K KIKWETE ASUBIRIWA KUTAJA JINA LA MRITHI WA SAID MWEMA

 Ndugu Watanzania, juzi vyomba vya habari vilitoa habari na maelezo juu ya majina ya matatu yaliyopendekezwa kwa rais kikwete ili ateue mmoja wao kuwa IGP, leo tulitarajia kuona jina moja limetokea kati yao, lakini mapka sasa Rais amewapandisha vyeo maofsa wengine na kuweka kiporo suala la IGP, atunatarajia kabla ya week hii atakua amekata kiu ya watz wengi kutaka kumjua mteule mpya ni nani...soma hapa chini ujue majina ya waliopandishwa vyeo.
NOV 21
Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Jeshi la Polisi Nchini:Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama amewapandisha vyeo maafisa 77 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP),Soma Majina Yao


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa 77 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).


Miongoni mwa maafisa waliopandishwa vyeo kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ni pamoja na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Engelbert Kiondo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala ACP. Marietha Minangi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ACP. Diwani Athumani na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Geofrey Kamwela.


Wengine ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP. Frasser Kashai, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP. Faustine Shilogile, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma ACP. David Misime, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ACP. Ferdinand Mtui, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP. Costantine Massawe, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita ACP. Leornad Paul, Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP. Ulrich Matei na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ACP. George Mwakajinga.


Zaidi ya hao wengine ni, Kamanada wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Evarist Mangala, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Deusedit Nsimeke, Kamanada wa Polisi mkoa wa Njombe ACP. Fulugence Ngonjani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari na baadhi ya Makamanda wa vikosi, Wakuu wa vitengo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar Es salaam.


Kufuatia kupandishwa vyeo kwa Maafisa hao wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema, amemshukuru Rais wa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.


Aidha, IGP Mwema amewapongeza wale wote waliopandishwa vyeo, na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika kuimarisha Usalama wa raia na mali zao kwa kuwa cheo ni dhamana.


Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa jeshi la polisi

No comments:

Post a Comment