Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, January 12, 2014

MAPUMZIKO: Kesho, Jumatatu (13/01/2014) na Jumanne (14/01/2014) ni sikukuu za Mapinduzi ya Zanzibar na Maulid.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Shein ametangaza kuwa kesho Jumatatu, Januari 13, 2013 itakuwa siku ya mapumziko ya kitaifa kwa Zanzibar kwa ajili ya kuadhimisha na kusherehekea kumbukumbu ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Baadaye, Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete alitangaza pia kuwa kesho itakuwa siku ya 
mapumziko kitaifa kwa Tanzania Bara, hivyo kuifanya Tanzania nzima kuwa mapumzikoni.

Tangazo ilililotolewa na Baraza Kuu la Waisalam Tanzania, BAKWATA limetangaza kuwa kesho usiku yatafanyika maulid ya kuadhimisha mazazi ya Mtume (S.A.W).

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa BAKWATA, Kitaifa maulid itasomwa Kigoma Mjini baada ya Swala ya I’sha.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Baraza la Maulid litafanyika saa tisa alasiri (9.00) mjini Kigoma siku ya Jumanne, tarehe 14 Januari 2014 ambapo pia itakuwa siku ya mapumziko.

TAARIFA RASMI YA IKULU KWA  UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.               

Naye Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar  katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.

Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.

Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.               

Naye Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.

Mwisho.
Imetolewa na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
Dar es Salaam.
12 January, 2014
Source: wavuti

No comments:

Post a Comment