Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, January 4, 2014

WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KADHAA KUJERUHIWA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI/NGEMA

Wananchi wakiwa katika eneo la machimbo ya moramu.

Watu wawili wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi/ngema katika eneo la Mlima Terati lililopo halmashauri ya jiji la Arusha wakati wakiwa wanapakia moramu kwenye gari aina ya Isuzu lori juzi saa 3:30 asubuhi.

Mmoja kati ya marehemu hao ametambulika kwa jina la Joseph Solomoni huku mwingine bado hajafamika mara moja.

Ajali hiyo mbaya iliyotokea tarehe 2 Januari 2014 ni ajali ambayo imetokea ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu kufariki dunia kwa watu 13 katika machimbo ya Moramu yaliyoko Moshono jijini Arusha ambapo viongozi mbalimbali wa mkoa na sekta ya madini walitoa amri kufungwa kwa machimbo yote yasiyokuwa na kibali wala kufuata sheria za machimbo.

Tukio hilo lililoshtua watu wengi limezua minong'ono kuwa "Je tamko la viongozi hao ilikuwa zuga ya huzuni ya ndugu wa marehemu walioufariki siku chache zilizopita....au ilikuwa siasa za kujitafutia umaarufu?"

Tukio hilo lililokuwa kama janga la kitaifa si la mkoa pekee bali viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dola waliahidi kulifuatilia na vioozi wengi walitoa matamko mbalimbali kwa kukagua machimbo yote huku naibu Waziri wa madini Masele akiahidi pia kulivalia njuga. Na kuhakikisha kuwa tatizo kama hilo halitajitokeza tena katika eneo hilo la machimbo ya moramu. 

Lakini chakushangaza haujapita hata muda mrefu tatizo limeena watu wawili kuangukiwa na kifusi/ngema. Chakujiuliza je utendaji wa viongozi wetu wa kuwatumikia wananchi na kuwalinda ni nguvu ya soda pindi tu inapofunguliwa gesi hutoka kwa kasi na kutulia baada ya mda mfupi ndivyo na utendaji ulivyo kuwa unashughulikiwa kwa maneno pale janga linapotokea ili kujizolea umaarufu na kujiweka katika nafasi nzuri katika jamii?

 

wakazi wa eneo hilo wakiangalia eneo hilo kwa masikitiko.

Blog hii inaahidi kulifuatilia tukio hili na kujuza muendelezo wake pamoja na matamko ya viongozi yatakayotolewa na viongozi mbalimbali juu ya tukio hilo, ukiachilia mbali lile lililoua watu 13 Moshono.
Chanzo: Berthamollel Blog

No comments:

Post a Comment