Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, March 24, 2014

WANAFUNZI WAWILI WA CHUO CHA MWENGE MOSHI WATUHUMIWA KWA UBAKAJI..,

Katika jambo ambalo limevuta hisia za wanafunzi wengi na walimu wa Chuo cha Mwenge ni Tukio lililotokea leo Majira ya Jioni hii katika Chuo cha Mwenge kilichopo Moshi.

Kwa Mujibu wa mzazi wa watoto wanaotuhumiwa kubakwa   alieleza tukio zima kuwa siku ya ijumaa majira ya Jioni Binti yake (Jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 15 na ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Maki Sekondari iliyoko Olele huko Marangu Kitowo alitoweka nyumbani Huko Marangu Kitowo akiwa na mwenzake (jina la Jina linahifadhiwa) mwenye umri wa Miaka kumi na sita na hawakuweza kuonekana mpaka jumapili jioni. Baada ya kuonekana ndipo walipobanwa na kusema walikua Moshi mjini kwa Mwanaume ambaye alikua ni mwalimu wao shuleni na anasoma chuo cha Mwenge.


Afisa wa Polisi anayeshughulikia Dawati la Jinsia na Watoto Afande Kasusura akiwa amemkamata Mtuhumiwa mmoja aitwaye Majaliwa nje ya chuo cha Mwenge.

Baada ya maelezo ya watoto ha Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Wazazi wa watoto hao ndipo walipofika  katika chuo hicho na kuweza kuwatia mbaroni wanafunzi hao mdugu Sebastian Mashauza Mwenyeji wa Kigoma na ni mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza  na Mwenzake alitambulika kwa jina moja la Majaliwa Mwenyeji wa Kigoma na ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho.

Mtuhumiwa akioneshwa watoto alioshiriki kuwabaka waliopo ndani ya Gari kabla ya kwenda kuonesha mwenzake alipo.

Mmoja wa waathiriwa  akizungumza na muandishi wetu alisema Anamtambua Sebastian Mashauza kama mwalimu wake alikuja shuleni kwao akawa anawafundisha somo la Kiswahili, Baada ya mwezi mmoja aliondoka wakawa wanawasiliana kwa njia ya simu na siku ya ijumaa ndio mwalimu huyo akamtumia shilingi elfu kumi kwa njia ya M Pesa ili aje mjini na akamwambia aje na mwenzake ndipo alipomuomba Rafiki yake Kresta amsindikize na walipofika ulipofika usiku Mwalimu huyo akamshawishi walale ndipo amwalimu huyo alipomwambia Kresta alale na Rafiki yake aitwae Majaliwa.  Mwanafunzi huyo alizidi kusema kuwa walipotaka kuondoka siku inayofuata hawakupewa nauli ndipo ikapelekea walale tena mpaka siku ya jumapili walipopewa nauli na kuondoka kurudi nyumbani.

Afande Kasusura akimpeleka Mtuhumiwa kuonesha mwenzake alipo.

  Hata hivyo uchunguzi wa awali umebaini kuwa Sebastian Mashauza alifundisha katika shule ya Maki sekondari anayosoma Mmoja wa wanafunzi hao na alikua kama mwalimu wa field hapo kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kwa sasa watuhumiwa wako Kituo cha Polisi cha Marangu tayari kwa kusubiri Utaratibu wa kisheria kukamilika kabla ya kupelekwa Mahakamani.

Majaliwa akitolewa ndani ya nyumba wanayoishi na ndio nyumba iliyotumika kuwabaka watoto hao baada ya mwenzake kupatikana


Mtuhumiwa namba moja Sebastian Mashauza mwalimu aliyewarubuni wanafunzi wake akiwa chini ya ulinzi mkali.

No comments:

Post a Comment