Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, June 18, 2014

JAMII YA KIMASAI WILAYANI MWANGA WANAHITAJI MAJI SAFI NA SALAMA

MWANGA serikali imetakiwa kutambua uwepo wa jamii ya kimasai na kuwapelekea mahitaji muhimu kama maji hospital na shule, ili nao waweza kuishi maisha ya kawaida kama watanzania wangine hapa nchini.

Hayo yalisemwa jana na kiongozi mila wa jamii ya kimasai Leguna olebulu Joshua, alieteuliwa na wazee wa jamii ya kimaasai ambae ataongoza rika la vijana wa jamii hiyo wa mkoa wa kilimanjaro na tanga, ambapo alisema atahakikisha jamii hiyo inapata mahitaji muhimu kama elimu na hospitali na kuondokana na kutumia miti shamba.

Alisema katika kijiji cha karamba kwenye kitongoji cha toloha, hawana maji safi na salama na kwahiyo wanalazimika kutumia masalia ya maji ya mvua zilizonyesha na kutwama kwenye madimbwi.

“Sisi hutujawahi kunywa maji safi na salama katika kijiji chetu huwa tunakunywa maji ya yiliyotwama kwenye madimbwi baada ya mvua kunyesha, na hayo ndiyo tunayotumia kwa ajili ya mifugo pia.”

Alisema maji hayo ambayo ni tope ndio wanayotumia wananchi wanaoishi katika kijiji hicho na kwamba maji hayo yakiisha wanalazimika kutembea siku nzima ili wapate maji ambapo wanayachukuwa katika ziwa chale lililopo mpakani mwa Kenya na tanzania.
“Tunaomba serikali ituangalie na sisi pia ni binadamu kama wengine  na tuna mahitaji kama binadamu pia watuchimbie hata maji ili tuweze kupata  maji safi na salama” alisema Joshua.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha karamba  kata ya Toloha wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Kishingo kimatonge,  alisema kero kubwa katika kijiji hicho  ni ukosefu wa maji safi na salama  na kwamba wamekuwa wanatumia maji ya  yaliyotwama.

“Kweli sisitumeshazoea kutumia maji hayo , ila serikali ingeona umuhimu wa kutuwekea maji safi na salama kwa kuwa tunateseka sana kipindi cha kiangazi kwa kuwa tunaenda mbali kuchukua maji” alisema Kimatonge

No comments:

Post a Comment