KILIMANJARO kufuatia kero ya miaka mingi ya wadau wa usafirishaji wa abiria na
mizigo mkoani kilimanjaro katika mizani ya Njiapanda ya Himo wilayani Moshi
imeondolewa baada ya wakala wa barabara mkoani Kilimanjaro (TANROAD)
kukamilisha ujenzi wa mizani mpya katika barabara kuu inayotokea Moshi kuelekea Dar es salaam.
Wakizungumza na muandishi wa mtandao huuj ana baadhi ya wadau wa usafirishaji walisema kuwa kabla ya
kujengwa kwa mizani hiyo walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kupoteza muda
mrefu katika foleni ya kupima uzito katika mizani ya mwanzo.
Hata hivyo wadau hao Francis Ali, Salum Awadhi, na Wilton Meena walisema
kujengwa kwa mizani hiyo kutaondoa kero
mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili ikiwa ni pamoja kukaa kwa muda mrefu
katika mizani hiyo bila kupatiwa huduma ya kupimimwa uzito kwa magari yao.
Aidha walisema kuwa kuna
haja ya kuiongezea uwezo barabara hiyo ambayo hupitisha magari mengi ya ndani na nje ya Tanzania kwa kuwa mizani mpya ni ndogo na haiwezi
kukithi mahitaji
Mizani hiyo imeanza kutumika mwanzo mwa mwenzi Julai Mwaka 2014
ambapo magari yote yanayo toka Dar es salaam na Tanga yanapima uzito katika
mizani mpya na yale yanayotoka Arusha, Moshi na nchi jirani kupitia Namanga na
Mombasa yanapima uzito wake katika mizani
ya zamani.
Kwa upande wake Meneja wa TANROAD mkoani Kilimanjaro Marwa Rubrya
alisema, mizani hiyo mpya imegharimu fedha nyingi sana, baada ya
kilio cha muda mrefu cha usafirishaji na abiria wakiwemo wafanyabiashara.
Nae afisa wakala wa vipimo mkoani Kilimanjaro Efremu Asenga, alithibitisha
ubora wa mizani hiyo mpya baada ya kuifanyia tathmini ya vipimo kitaalamu ili
kuondoa malalamiko ya kuzidishiwa uzito yaliyokuwa yakitolewa na wamiliki na
madereva wa magari hayo.
Afisa wa zamu wa mizani ya zamani Abubakari Makoi alisema kuwa,
idadi ya magari yaliyopimwa katika mizani hiyo kwa kipindi cha wiki tatu za
mwezi julai yalipungua kutoka 7509 wakati kabla ya mizani hiyo mwezi juni
katika kipindi hicho magari 15,242.
No comments:
Post a Comment