MOSHI kibaka
wa uporaji kwa kutumia nguvu vitu mablimabali katika nyumba za watu ameuwawa
kikatili na watu wasiojulikana kwa kupigwa mawe kichani katika mtaa wa kaloleni, kata ya Pasua, manispaa ya
Moshi, Mkoani kilimanjaro.
Kamanda wa
polisi mkoani Kilimanjaro Robert boaz, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
julai 24 mwaka 2014 majira ya saa 1:00 kamili asubuhi wapita njia walikuta
mwili huo metelekezwa ndipo wakatoa taarifa polisi.
Boaz alisema
kuwa kijana huyo ametambulika kwa jina
moja la Alen (25) maarufu kwa jina la Mmeruu na kwamba
alikuwa anatafutwa na jeshi la polisi kwa muda mrefu kutokana kupora watu kwa
nguvu vitu mbalimbali.
Alisema mwili
huo ulikuwa na majeraha makubwa kichwani, na damu nyingi zikiwa zimevuja, huku
pembeni ya mwili huo kukiwa na mawe makubwa ambayo yalitumika kumjeruhi marehemu
“Uchunguzi
unaendelea ili kuweza kubaini chanzo cha kifo cha marehemu ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua
waliofanya kitendo hicho cha kinyama”alisema Boaz.
Mwili wa
marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Mawezi kamanda amewataka
ndugu na jamaa kwenda kutambua mwili huo.
No comments:
Post a Comment