Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 15, 2014

WAZAZI WATAKIWA KUWA WAZALENDO KATIKA KULIPA ADA KWA AJILI YA WATOTO WAO

HAI wananchi wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuwa wazalendo wa katika kulipa ada ya shule kwa watoto wao ili kuwapa watoto fursa ya kupata elimu kama ilivyo kusudiwa.

Swala hilo muhimu liliongelewa na Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Hai, Bw. Julius Kakyama, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya kibaoni kwenye kikao kilicho fanyika hivi karibuni katika ofisi ya mtaa wa kibaoni kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi.

Kakyama alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiwapeleka watoto wao shuleni kwa lengo na kusoma lakini likija suala la kuchangia chakula mashuleni wamekuwa wakaidi sana, jambo hilo la kutokutaka kutoa michango ya shule linarudisha elimu nyuma, hivyo amewaomba wazazi wilayani humo kuchangia chakula  kwa wingi mashuleni ili wanafunzi waweze kufaulu, kwani wanafunzi kukosa chakula  kunawafanya kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.

Alisema kuwa anatambua mchango mkubwa toka serikalini wa ujenzi wa shule na mabweni kwa shule ya sekondari Hai Day unaoendelea kufanyika pamoja na juhudi za wananchi katika kutoa michango yao kufanikisha ujenzi huo.

Akizungumzia suala la maabara katika shule ya sekondari Boma alisema kuwa wametoa ushirikiano katika ujenzi kwa fedha za TASAF  mwaka 2007 na kukamilisha madarasa.

Ameongeza pia mwaka 2011 walitumia fedha zilizo tolewa na TASAF na kujenga vyoo vya shule ambapo pia vilikamilika na kusema kuwa katika suala la ujenzi wa  maabara kuna mpango unaoandaliwa na halmashauri ya kuandika barua kwa watendaji kata ili waweze kufanyia mchakato suala hilo la ujenzi wa maabara.

No comments:

Post a Comment