ROMBO
wanafunzi wawili wa shule wa ya sekondari ya Makiidi iliyopo wilaya ya
Rombo mkoani Kilimanjaro, wanashikiliwa na Jeshi polisi mkoani
Kilimanjaro kwa tuhuma za kubaka mwanafunzi wa shule ya msingi Maureni
iliyopo Mkuu wilayani Rombo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Makiidi, Rogath Namfua alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kwamba alisema lilitokea Septemba 5 mwaka 2014
majira ya saa sita mchana na kwamba wanafunzi hao walimvamia mwanafuzi
wa shule ya Msingi Maureni ambaye anasoma darasa la pili na kumbaka.
Namfua alisema wanafunzi hao walimvamia mwanafuzi huyo wa darasa la pili
wakati akirudi kutoka shuleni na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama.
“Walimvamia mtoto huyo na kumpeleka shambani na kumfanyia kitendo hicho
cha kinyama mwanafunzi huyo wa darasa la pili na kumuumiza vibaya sehamu
za siri” alisema mwenyekiti huyo.
Alisema mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Huruma na kupatiwa
matibabu na kwamba kwa sasa yupo nyumbani anaendelea na dawa.
Mwenyekiti huyo alisema baada ya kuthibitika kuwa mwanafunzi huyo
aliingiliwa na wanafunzi hao walikamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi
cha wilaya ya Rombo.
kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kwamba wanafunzi hoa wanashikiliwa kwa uchunguzi
zaidi.
No comments:
Post a Comment