Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 30, 2014

Wananchi wakumbushwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura

KILIMANJARO mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, Bw. Melckzedik Humbe amewakumbusha wananchi wote wa wilaya ya Hai wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwani muda umemalizika.

Hayo yalisemwa jana na mkurungenzi huyo katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Humbe alisema wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kwa hizi siku tulizoongeza za wiki moja kwani mwisho wa kujiandikisha kwenye daftari hilo ilikuwa jana tarehe 29 septemba 2014.
 
Tulikubaliana na kuongeza wiki moja ili wananchi wapate fursa ya kujiandikisha na muda ukifika waweze kupiga kura na kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwakani 2015.

Alifafanua kuwa shughuli hiyo itawahusu wananchi wote wenye sifa na walio na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea na kwamba kama mwananchi yoyote hatajiandikisha kujisajili kwenye  daftari hilo atakosa haki zake za msingi ikiwemo kukosa kitambulisho cha Taifa.

Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo Clement Kwayu alisema mpaka sasa katika wilaya hiyo ni kata tano ndiyo  zimewasilisha majina ofisini hapo halmashauri kati ya kata kumi na nne jambo ambalo litakuja kumfanya mwananchi apoteza haki zake kwa kutokujiandikisha.

Hivyo ameomba wenyeviti wa vitogoji, wenyeviti wa vijiji, watendaji pamoja na madiwani kushiriki kwa pomoja kwa hizi siku chache kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari hilo.

No comments:

Post a Comment