Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 17, 2014

Waziri wa nchi ofisi ya raisi Dkr. Mary Nagu awataka wafanyabiashara kuacha kupita njia za panya

KILIMANJARO waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Mary Nagu, amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuacha tabia ya kutumia njia za panya pindi wanaposafirisha mizigo yao, na badala yake amewataka kuvitumia vituo vilivyojengwa mipakani ili kuweza kusafirisha mizigo hiyo.

 Dkt. Nagu ameyasema hayo, wakati alipotembelea jengo la kutoa huduma kwa pamoja, (one stop border), lililojengwa eneo la Holili wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro.

Alisema  lengo la kujengwa kwa kituo hicho kitarahisisha uingizwaji na utoaji wa mizigo kwa haraka na kwamba wafanya biashara wa Tanzania ni vyema wakashirikiana  na wenzao wa nchi za jirani ili kukuza biashara zao.

 Dkt. Nagu alisema Tanzania ni moja kati ya nchi ambayo ina gharama kubwa sana katika kufanya biashara, hali inayochangia  wawekezaji kutofikiria kuwekeza hapa nchini.

Hata hivyo waziri huyo amepongeza ujenzi wa kituo hicho cha Holili na kudai hatua ilipofikia inatia matumaini kwani vituo vingi vya mipakani upande wa Tanzania vilikuwa katika hali mbaya na kwamba uwepo wa kituo hicho kutasaidia kupunguza gharama hivyo kuwavutia wafanyabiashara wengi zaidi kuja kuwekeza hapa nchini.

 Kwa upande wake kaimu mkuu wa kituo cha forodha Holili, Nassor Salim Juma, alisema kuwa kukamilika kwa kituo hicho kunakotarajiwa kufanywa hivi karibuni kutasaidia kurahisha kazi na kwamba linatarajiwa kutumika kama linavyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment