Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 10, 2014

Askari jijini Arusha wafanikiwa kumua jambazi anayetuhumiwa kuwauwa baadhi ya wanawake

 
Picha ya juu na chini wakazi wa jiji la Arusha waliojitokeza kuuangalia mwili wa jambazi alieuwawa na polisi usiku wa kuamkia leo, anayetuhumiwa kuwauwa baadhi ya wanawake jijini Arusha.



Picha ya juu na chini ni mwili wa Jambazi huyo ukiwa umelazwa ndani ya gari la polisi mara baada ya kuwawa tayari kwa ajili ya kupelekwa mochwari.



Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wakiendelea kushuhudia mwili wa jambazi huyo nje ya jengo la makao makuu ya polisi mkoani Arusha.







Baadhi ya silaha zilizokutwa nyumbani kwa mtu huyo anadhaniwa kuwa ni jambazi.


kamanda wa polisi akionesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina la "G lock Fab Defence" moja ambacho jambazi huyo alikuwa akitumia.

Jambazi mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan Abudallah alimaarufu kwa jina la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa Moivo ameuwawa baada ya kupigwa risasi katika majibizano na askari wa jeshi la polisi.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa tukio hilo limetokea October 10 mwaka huu majira ya saa nane na dakika nne usiku katika kijiji cha Moivo kilichopo ndani ya kitongoji cha Enaboishu wilayani Arumeru.

Alisema kuwa marehemu Ramadhan Abdallh aliuwa anatafutwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo yameshawahi kutokea ndani ya mkoa huu pamoja na katika maeneo mbalimbali ya nchi hiii.

Alibainisha kuwa kuuwawa kwa jambazi huyo kumetokana na juhudi na kutumia mbinu za kisasa za kiupelelezi na kufika nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu) ambapo askari polisi walimwamuru ajisalimishe lakini alikaidi amri na kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha askari kujibu mashambulizi na kumsababishia umauti kumfika.

“Mara baada ya kumpiga jambazi huyo polisi walianza kumpekuwa mwili wa marehemu na alipatiana akiwa na bastola aina ya "G lock 19" yenye namba "RLU976" iliyotengenezwa nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14) ambapo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano ya risasi na mbali na hapo polisi pia walifanya upekuzi katika chumba cha mtu huyo anayesadikika kuwa ni jambazi na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na magazine zingine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja, Radio call moja yeye nembo ya ITSS/UNICTR pamoja na pikipiki aina ya toyo power king rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU pamoja na kofia ngumu”alisema Sabas.



Aidha alibainisha kuwa pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya mtu huyo anayesadikika kuwa ni jambazi pia walifanikiwa kupata pingu moja, plate namba ingine ya pikipiki yenye namba za usajili T 805 CVD ambapo alibainisha kuwa mtu huyo anayesadikika kuwa ni jambazi alikuwa akibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara pamoja na chombo maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla yakupiga risasi (G lock Fab Defence moja),kifaa cha kusafishia bastola pamoja na koti kubwa jeusi. 


Kamanda Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo mtu huyo anayesadikika kuwa ni jambazi alishayafanya kuwa ni pamoja na tukio lililotekea Augast 6 majira ya saa tatu na nusu usiku maeneo ya kwa iddi ambapo mtuhumiwa akiwa na mwenzake ambaye ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke aliyefahamika kwa jina la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina wakati akijiandaa kuingina nyumbani kwake, huku tukio lingine likiwa limetokea Augast 21 saa 19:00 maeneo ya olasiti ambapo mtu huyo anayesadikika kuwa ni jambazi akiwa na mwenzake kwenye pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi ya mdomo na kutokea kichwani mototo aitwaye Christen Nikson, mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, na baadae majeruhi kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu. 


Kamanda Sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuwahaidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi na kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.

“Arusha sio sehemu ya kuifadhi wahalifu ivyo tutajitaidi kwa hali na mali kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote na napenda kuwaaambia wahalifu waache mapema maana sasa ivi tumejipanga vilivyo ,pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia waendelee kuwafichua wahalifu popote pale ili tuwaangamize kabisa” alisema Sabas.



Mmoja wa wananchi ambaye alijitokeza kushuhudia maiti ya jambazi hilo Aliyejitambulisha kwa jina la Alaija Saro akiongea na libeneke blog hili alilipongeza jeshi la polisi kwa kuweza kumuangamiza jambazi hilo kwani limekuwa likiwatia mashaka watu wengi na kuwanyima raha kwa jinsi walivyokuwa wanauwa watu.

Chanzo: woindeshizza blog

No comments:

Post a Comment