Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, October 25, 2014

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro awahakikishia wananchi kuwa Ebola haijafika KilimanjaroKILIMANJARO wakazi wa kata ya Shirimatunda Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamekumbwa na hofu kubwa, baaada ya kufungwa kwa zahanati ya kata hiyo kwa hofu ya kumhudumia mgonjwa anayedaiwa kuwa na virusi vya ugonjwa hatari wa Ebora.

Wakazi hao wameanza kuhamisha familia zao  kwa hofu ya kukumbwa na ugonjwa,  ambao tayari umekwisha kuua mamia ya watu katika baadhi ya nchi za Kiafrika na Marekani.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amewaondoa hofu wakazi wa mji wa moshi na mkoa wa Kilimanjaro, kutokana na taharuki iliyoukumba mkoa wa Kilimanjaro hususani mji wa Moshi, ya kuwepo kwa mgonjwa anayehisiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ebora.


Gama alifafanua kuwa mgonjwa huyo ambaye ni mzaliwa wa Marangu wilaya ya Moshi ambaye makazi yake yako jijini Dar es Salaam, alifika mkoani Kilimanjaro akitokea Dar es Salaam na alionekana kuwa na homa kali ambapo alitengewa eneo maalumu la matibabu.

Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Mtumwa Mwako, amesema kituo cha Shirimatunda kimewekwa kwa ajili ya tahadhari ya watu wanaohisiwa kuwa na Ebora.

No comments:

Post a Comment